Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dr. Vincent Mashinji amesema sharti la kuripoti kituo
Kikuu cha Polisi Central ni gumu kulingana na kazi wanazozifanya.
Dr.
Mashinji ameyasema hayo leo April 20, 2018 baada ya yeye na Viongozi
wenzake wa chama hicho kuripoti kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya sharti
la dhamana walilopewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Dr. Mashinji amesema, “Iliamuriwa na mahakama
kila siku ya Ijumaa turipoti kwa RPC hapa Central Polisi ikiwa kama
sehemu ya sharti la dhamana tulilopewa mahakamani kwenye ile kesi yetu
inayojumuisha watu 9”
“Kimsingi
ukiangalia ni sharti gumu kwani nature ya kazi zetu inatutaka kusafiri
kwenda kujenga chama, hivyo tunashindwa ila kwa vile ni amri ya mahakama
lazima tutekeleze kwani ndio inatenda haki,” -Dr. Mashinji.
Pia Dr. Mashinji amesema kama mahakama itaridhia kuwaondolea sharti hilo itawasaidia sana.



No comments:
Post a Comment