Mbunge
wa Chalinze kupitia CCM, Mh. Ridhiwani Kikwete ameonesha kuridhishwa na
kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli hususani katika kuboresha miundombinu nchini.
Ridhiwani
ameyasema hayo baada ya kujionea ub ora wa daraja la Kelema wilayani
Chemba mkoani Dodoma, alipopita eneo hilo ikiwa ni sehemu ya safari yake
kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Muungano yaliyofanyika jijini
humo.
Kupitia
mtandao wa Twitter Mh. Ridhiwani ameandika, ''Nikiwa na mke wangu,
kuangalia uzuri wa nchi yetu. Hakika ni nchi nzuri yenye kuvutia.
Hongera sana Rais wangu @MagufuliJP kwa kusimamia Miundombinu, pia
Asante @WorldBankAfrica kwa kusaidia maendeleo''.
Aidha
katika ujumbe huo wa Ridhiwani pia ameishukuru Benki ya Dunia kwa
misaada inayotoa hususani ujenzi wa barabara ambao ndio umekuwa
kipaumbele chake katika nchi zinazoendelea ikizisaidia kwa mikopo ya
masharti nafuu.
April
27 Rais Magufuli alizindua barabara ya Kondoa-Babati, yenye urefu wa Km
251. Katika uzinduzi huo aliwataka wananchi kutunza miundombinu hiyo,
haswa alama za barabarani kwani hiyo ndio barabara kuu kwa upande wa
Kaskazini.




No comments:
Post a Comment