Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia
kufanya ziara ya kikazi mkoani Iringa kuanzia leo tar 29 mwezi huu
hadi tar 4 mwezi ujao.
Hayo
yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kuwa wanatarajia
kumpokea rais Dkt. Magufuli leo tar 29 mwezi huu.
Alisema
kuwa mara baada ya kupokelewa Rais Dkt. Magufuli atazindua barabara ya
kijiji cha Migori kwenda Fufu kupitia Iringa mjini.
“Siku
ya Mei Mosi Rais Dkt. Magufuli atakuwa mgeni rasmi, ambapo kitaifa
yatafanyika mkoani hapa ambapo kutakuwepo na viongozi mbalimbali akiwemo
Waziri Mkuu, Spika wa bunge na viongozi wengine,”alisema Masenza
Mkuu
huyo wa mkoa wa Iringa amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika
maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi ambapo zimepangwa kufanyika mkoani
humo.
Hata hivyo, ameongeza kuwa Rais Magufuli akiwa ziarani mkoani humo atazindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo vikiwemo viwanda.



No comments:
Post a Comment