
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la maji safi na salama lenye uwezo wa kubeba lita laki mbili na nusu (lita 250,000) lililopo Kikwajuni kwa Mselem ambapo watu elfu saba na mia tano (watu 7,500) watanufaika.
Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kuwa na Kamati ya Maji mara baada ya mradi huo kukamilika na kuwataka wananchi hao kuchangia huduma ya maji ili waweze kuendesha mradi huo.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu wawapeleke watoto wao kwenye vituo vitakavyoweza kuwafundisha mambo mbali mbali badala ya kuwafungia ndani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo ya ujenzi wa miundo mbinu katika mradi wa maji utakao
nufaisha wakazi wa elfu saba mia tano (7500) katika Shehia 4 mara baada
ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la maji safi Kikawajuni kwa
Mselem katika jimbo la Kikwajuni, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi
Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la watu wenye ulemavu Shauri Moyo, Mikunguni.
Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo na kukagua miradi ya Chama Cha Mapinduzi Unguja, Zanzibar.


No comments:
Post a Comment