
Wito ulitolewa jana wilayani Kishapu na Wakuu wa Mikoa ya Shinyanga Zainabu Telack na Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya upandaji miti Kitaifa.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tanzania ya Kijani Inawezekana , Panda Miti kwa Maendeleo ya Viwanda.
Telack alisema kutokana na ukataji wa miti ovyo Mkoani Shinyanga hivi sasa unapata mvua ambayo ni sawa ruzuku ambapo hadi maeneo mengine yanayowazungua yawe na mvua nyingi ndipo Mkoa huo nao upate mvua.
Alisema ukosefu wa mvua za kutosha umekuwa ukiathiri hata mifugo kwa sababu ya ukosefu wa nyasi kwa ajili ya malisho kwa kuwa hakuna miti ambayo ingesababisha unyevunyevu ardhini.
Telack alitoa wito kwa wataalamu kuangalia uwezekano kutengeneza majiko kwa wingi ambayo yatapunguza matumizi ya mkaa na kuni na hivyo kuanzisha matumizi ya pumba za mpunga kwa ajili ya upikaji na hivyo kupunguza ukataji miti ovyo kwa ajili ya nishati ya kupikia.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga aliwashauri Wachimbaji madini wadogo kuanza kufikiria matumizi ya vyuma ili kujengea mashimo ya uchimbaji kwa ajili ya kuepusha ukataji wa miti ovyo na hivyo kuharibifu mazingira.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwata wadau mbalimbali kuwajibika katika nafasi yake ili kuhakikisha hakuna mtu anayekata mti bila kuwa na kibali na hivyo kusababisha uharibifu wa mistu asili na ile ya kupandwa.
Alisema kusipokuwepo na uwajibikaji wa pamoja katika kukabiliana na tatizo la ukataji miti ovyo upo uwezekano wa Mikoa ya Tabora na Shinyanga kuwa sehemu ya Jangwa na hivyo wakazi wa eneo hilo kulazimika kuondoka.
Mwanri aliongeza kukishageuka Jangwa hakuna tena maendeleo kwani hakuna Mwekezaji atakayekuja kuwekeza katika eneo ambao halina maji na wala watu hawaishi.
Aliwataka watendaji wote kuanzia ngazi ya Shina hadi Mkoa kuhakikisha wanasimamia Sheria zote ambazo zinazuia mifugo kuzurura ovyo, uvamizi wa vyanzo vya maji , ukataji miti ovyo ili kuokoa mistu iliyopo na miti inayoendelea kupandwa.
Naye Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Valentine Msusa alisema kuwa kila mwaka uharibifu wa misitu unapoteza ekari 372,000 kila mwaka ambayo baadhi yake ni mali ya Serikali kuu, Halmashauri, Vijiji na binafsi.
Msusa alisema kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo Kanda ya Magharibi katika mwaka ujao wa fedha inatarajia kuimarisha bustani katika vituo mbalimbali ikiwemo Kakonko Kibondo, Tanganyika, Mpanda, Mlele kwa ajili ya kuotesha miche ya miti ya aina mbalimbali kwa ajili ya upandaji.


No comments:
Post a Comment