Majambazi wanne wameuawa na polisi asubuhi ya leo Ijumaa Aprili 20, wakati wakijaribu kupora Kisarawe mkoani Pwani.
Kabla ya kuuawa yalitokea majibizano ya risasi kati yao na askari Polisi.
Imedaiwa
majambazi hao wametokea jijini Dar es Salaam na walikuwa wanatumia gari
lenye namba za kibalozi hatua iliyosababisha askari wa usalama
barabarani kutowahisi chochote kwani gari hizo sio rahisi kusimamishwa
ovyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Ulinzi na Usalama
mkoani Pwani, Evarist Ndikilo amethibitisha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment