Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa
mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini
amelifunga rasmi.
Hayo
ameyasema leo Aprili 20, 2018; Ikulu jijini Dar es Salaam alipozungumza
na waandishi wa habari huku akionya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa
macho wakiwamo waandishi wa habari.
Amesema
jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi
kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi
kulishtaki jeshi.
”Katika
maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na
kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote.”
Alipoulizwa
kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo
amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa
huru hawana hatia.”
Mkurugenzi
huyo amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha amani inakuwapo,”na
niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo
sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia.”
“Na
wanaosema wataandamana, waambieni wasifanye hivyo kwani wakiandamana
watakwenda kuwasilimulia familia yake,” amesisitiza Biswalo
Pia,
amevionya vyombo vya habari ambavyo vinavyoweza kuchangia uvunjifu wa
amani, hatua zitachukuliwa hivyo kuvitaka kuwa makini na kutimiza wajibu
wao kwa kufuata misingi ya taaluma yao.
No comments:
Post a Comment