Ile
rufaa inayomhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini
(TFF), Michael Richard Wambura, imesikilizwa jana kwa pande zote mbili
kukutana katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo mitaa ya Karume,
Ilala.
Kwa
mujibu wa Wakili wa Wambura,Emmanuel Muga, amesema pande zote mbili
zimemaliza vizuri kikao hicho na mambo yamekwenda sawia, kinachosubiriwa
tu sasa ni maamuzi ya Kamati ya Maadili kutoa hukumu.
Muga
ambaye anamtetea Wambura, ameeleza TFF wamesikiliza kwa umakini utetezi
wa Wambura vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na
mustakabali mzima wa kesi hiyo.
Wambura
alikata rufaa kupinga kufungiwa kujihusisha na soka baada ya TFF
kumfungia kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo
pamoja na makosa mengine.
Kamati ya Maadili itakaa na kuandaa rasmi na majibu ya hukumu juu ya rufaa hiyo iliyosikilizwa jana Jumamosi.



No comments:
Post a Comment