Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaja mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na
Shinyanga kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa sekondari.
Waziri
mkuu pia ameitaja mikoa ya Rukwa, Geita, Tabora, Singida na Simiyu kuwa
inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi.
Majaliwa
ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa ameitaja mikoa hiyo leo Jumatatu Aprili
2,2018 akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Magogo mkoani
Geita.
Mbio
za Mwenge zitakazohitimishwa Oktoba 14,2018 mkoani Tanga zinaongozwa na
kauli mbiu “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya
nchi yetu.”
Majaliwa
amesema Mkoa wa Tabora unaongoza kwa asilimia 9.7 ya wanafunzi watoro
wa sekondari ukifuatiwa na Geita (asilimia 8.1), Mtwara (asilimia 6.1)
na Shinyanga (asilimia 6.3).
Kwa
shule za msingi, Rukwa inaongoza kwa asilimia 3.2, ukifuata Geita
(asilimia 3.1), Tabora (asilimia 2.9), Singida (asilimia 2) na Simiyu
(asilimia 2).
“Kwa
jumla utoro wa wanafunzi wa sekondari ni mkubwa kuliko shule za msingi.
Naikumbusha mikoa yote niliyoitaja kuhamasisha wananchi wakiwamo wazazi
na walezi kuhusu umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni kwa
kutumia utaratibu wa sheria zilizowekwa,” amesema Majaliwa.


No comments:
Post a Comment