NA Mahmoud Ahmad, DODOMA
SERIKALI
imewataka wawekezaji na wadau mbalimbali kuachana na tabia ya
kulalamika serikali na badala yake watoe ushauri kwa serikali ni jinsi
gani ya kutatua changamoto mbalimbali.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Biashara Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Mijage
alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akifungua mkutano wa wadau na
wawekezaji wa pamba,bidhaa za nguo na mavazi katika ukumbi wa mikutano
wa Hazina mjini hapa.
Alisema
pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazokabiliana na wizara
hiyo lakini ni wakati wa wadau kutoa maoni yao ya kuishauri serikali
pamoja na kuisaidia ili iweze kufanikiwa badala ya kuendelea kulalamika.
Hata
hivyo alisema kwa kuzingatia kuwepo kwa sera ya serikali ya viwanda ni
wakati sasa wa waekezaji kujenga viwanda ambavyo vitaweza kuzalisha
malighafi ambazo zinazalishwa nchii badala ya kuuza malghafi hizo nje na
kununua bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.
Akizungumzia
zao la pamba alisema kwa kuwa wananchi na wakulima wamehamasishwa zaidi
kulima pamba katika maeneo ya ukanda wa pamba ni lazima pamba
inayozalishwa nchini isiuzwe nje ya nchi na badala yake ichakatwe na
kuzalisha nguo na nyuzi ambazo zinaweza kutumiwa na kuzalisha bidhaa
bora.
Kwa
upande wake mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro,Siriel Mchembe,
ameitaka serikali kuhakikisha inaweka mikakati ambayo inaeleweka kwa
lengo la kujua soko la pamba pamoja na bei ambayo itakuwa inamanufaa kwa
wakulima.
Akichangia
katika mkutano huo mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa amemwakilisha
mkoa wa Morogoro, alisema kwa sasa wananchi wamehamasishwa zaidi kulima
zao la pamba na kufikia hatua ya kuachana na kilimo cha mahindi hivyo
wanatakiwa kuhakikishiwa kama pamba yao itakuwa na soko la uhakika.
“Kwa
sasa wakulima wamehamasishwa sana kulima pamba imefikia hatua wapo
wakulima ambao wameachana na kulima mahindi wakijua kuwa pamba itakuwa
na bei nzuri, sasa ikitokea pamba ikaa haina soko au kuonekna ni chafu
je wakulima hao tutawaambia nini” alihoji mkuu huyo wa wilaya.
Naye
mkuu wa mkoa wa Mara Adam Kigoma Malima alisema haiweze, Mawaziri,
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na wetendaji wengine wakaishi kwa
kulalamika badala ya kutafuta suluhusho.
Alisema
suala la uwepo wa viwanda unatakiwa kuwa na mikakati ya pamoja nadala
ya kuishi kwa malalamiko na kukosa ufumbuzi na maazimio ya pamoja na kwa
hali hiyo haiwezekani pakawepo na maendeleo.



No comments:
Post a Comment