Waziri
wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema kuwa hadi kufikia Julai mwaka
huu, ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme katika mto Rufiji utakuwa
umeanza.
Ameyasema hayo leo Aprili 3, wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha kufua umeme Kinyerezi awamu ya pili.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Rais John Magufuli.
Dk Kalemani amesema mradi huo wa miaka mitatu utakamilika kwa wakati.
Amesema
hatua inayoendelea sasa ni kutafuta mkandarasi ambaye hadi kufikia
Julai atakuwa ameshapatikana kwa ajili ya kuanza kazi.
“Sasa
tunamuandalia mazingira ili akipatikana aanze kazi bila kikwazo,
tumemboreshea barabara na tumeshapeleka umeme,” amesema Dk Kalemani.
Akizungumzia
suala la umeme wa uhakika, Dk Kalemani amesema hadi kufikia mwishoni
mwa mwaka huu watakuwa wamekamilisha uimarishaji wa miundombinu.
“Umeme
upo mwingi wa kutosha na wa ziada, kinachofanyika sasa ni kuboresha
miundombinu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tutakuwa tumelikamilisha
hilo na umeme kupatikana wakati wote na katika majira yoyote,” amesema
Dk Kalemani.



No comments:
Post a Comment