WAZIRI
Mkuu, Kassim Majali, ameshauri Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Upendo
Peneza, kukaa na Waziri wa Fedha na Mipango na yule wa Tamisemi,
kushauriana njia bora ya kuhakikisha taulo za kike zinapatikana kwa bei
nafuu ambazo wanafunzi walioshindwa kwenda shule wakati wa hedhi
watazimudu.
Kauli
hiyo ya Majaliwa imekuja baada ya Pendeza kutaka kauli ya Serikali juu
ya kondoa kodi kwenye taulo hizo, akisema baadhi ya wanafunzi kutoka
kaya masikini wamekuwa wakishindwa kuhudhuria mawasomo wawapo kwenye
hedhi kwa sababu ya kushindwa kumudu taulo hizo za kujisitiri.
“Kwa
kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha inaondoa vikwazo vyote kwenye
elimu, na Waziri wa Tamisemi alishaelekeza zile Sh 10,000 na Sh 20,000
zinazopelekwa kama ruzuku kwa shule za msingi na sekondari zitumike
kununua taulo hizo, lakini ikizingatia fedha hizo ni kidogo, kwanini
sasa Serikali kwenye sheria ya fedha inayokuja isiondoe kodi kwenye
taulo hizi ili wanafunzi kutoka kaya masikini waweze kuzimudu,” aliuliza
Peneza wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Akijibu
swali hilo, Majaliwa alisema “Serikali ina utaratibu wake wa kuondoa
kodi kwenye bidhaa zinazoleta tija ikiwamo uliyoisema mheshimiwa Mbunge,
kwa kuwa serikali imeanza kutoa fedha kama ulivoeleza, Wizara ya fedha
na Waziri (Tamisemi) wataona namna mtakavyokaa kuona jinsi ya kupunguza
bei kwenye vifaa ulivyoeleza.”



No comments:
Post a Comment