KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, imesema mpaka kufikia Februari
mwaka huu, Serikali ilikuwa imetoa Sh bilioni 576.52 pekee kati ya Sh
trilioni 1.07 zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya Bajeti ya Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18,
huku bajeti ijayo ikiwa imepungua kwa Sh bilioni 171.6.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Peter Serukamba, akisoma maoni ya kamati yake baada ya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu, kusoma makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara yake, alisema
fedha hizo zilizotolewa ni asilimia 53 tu ja bajeti yote iliyopitishwa
na Bunge.
Alisema pia kati ya fedha zilizotolewa, Sh bilioni 190.75 ni za matumizi ya kawaida ya wizara.
“Uchambuzi
wa kamti umebaini fedha zilizotengwa kwaajili ya utekelezaji wa
shughuli wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18, ni kiasi kidogo amcho
hakiridhishi na kinyume na matarajio ya Mpango wa Bajeti ambao Bunge na
Serikali tulikubaliana,” alisema.
Kwa upande mwingine, bajeti ijayo ya wizara ya Afya imepungua kw Sh bilioni 171.6 ikilinganishwa na ile inayoishia Juni 30.
Akisoma
hotuba bungeni jana, Waziri Mwalimu alisema kwa mwaka wa fedha ujao,
wizara yake inaomba kuidhinishiwa na Bunge Sh bilioni 898.374
ikilinganishwa na Sh trilioni 1.07.



No comments:
Post a Comment