Serikali
ya Tanzania kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wabunge na
viongozi wengine kuacha tabia ya kuingiza siasa kwa watu wanaoishi
mabondeni kwa kuwatetea kutohama maeneo hayo jambo ambalo linawapelekea
kupata madhara pindi mvua kubwa zinaponyesha kama ilivyo sasa.
Waziri
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Aprili 19, 2018 Bungeni jijini Dodoma
kwenye kikao cha 13 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mbunge Abdalla Mtolea ambapo
alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuhakikisha madhara
yanayojitokeza katika jiji la Dar es Salaam na mvua kudhibitiwa?
"kupitia
Manispaa za jiji la Dar es Salaam na serikali yake kupitia wizara zake
zinazo mipango ya kuboresha miundombinu katika miji yetu katika makao
makuu ya mikoa na maeneo yote yale yanayokaliwa na watu wengi ikiwepo
DSM. Tunayo miradi sasa ambayo itaweza kuboresha miundombinu ikiwepo na
bonde la Msimbazi ambalo linaleta madhara mengi...
Mara
kadhaa tumeshuhudia mvua hizi zinapoleta madhara kwa wale walioko
mabondeni pamoja na serikali kuwaambia waondoke mabondeni tumekuwa
tukiingilia sana utendaji kwa kuingiza siasa za kuwataka watu wabaki
huku wengine wakijafanya wanawaonea huruma na kushindwa kutoka katika
mabonde kutokana na utetezi unaotoka kwa watu wenye mapenzi yao
binafsi", amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema..
"Nitoe
wito kama ambavyo tunaendelea kutoa wito na Waheshimiwa Wabunge kupitia
Bunge hili tuwasii watanzania na kuwataka wote wanaoishi mabondeni
wahame kwasababu mvua hizi zinapokuja wanapata madhara makubwa na
hatimaye sasa hata katika kuwaokoa inakuwa shida. Kwa hiyo ni vizuri
sasa tukashirikiana".
Pamoja
na hayo, Majaliwa ameendelea kwa kusema "serikali kwa upande wake
inaanda fedha kuhakikisha kwamba ile miundombinu ya mabonde ina boreshwa
ili maji yaweze kupita kwa ulaini. Lakini watu waliokaa katika mabonde
na yale maeneo yote waliyokataziwa waanze kuondoka mapema ili wasiweze
kupata madhara pindi mvua nyingi zinapojitokeza".
Kwa
upande mwingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa pole wananchi wote
walioweza kupata maafa ya aina yeyote yaliyosababishwa na mvua
zinazoendelea kunyesha nchini



No comments:
Post a Comment