Wanamuziki
Nguza Viking maarufu Babu Seya wanawe Papii Kocha na Francis Nguza, leo
wamealikwa Bungeni na kuhudhuria kikao cha Bunge leo.
Mara baada ya wasanii hao kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, ukumbi wa Bunge ulilipuka kwa kuwashagilia.
Babu
Seya na wanawe hivi karibuni baada ya kutoka jela December 9, 2017 kwa
msamaha wa Rais, wamekuwa wakialikwa sehemu mbali mbali za serikali,
ikiwemo Ikulu na sehemu zingine za umma.
Babu
Seya na wanawe walihukumiwa kifungo cha maisha kwa tuhuma za kulawiti
na kubaka mwaka 2004 , na hatimaye neema ya Mungu kuwashukia pale Rais
John Pombe Magufuli kuamua kuwasamehe na kuwaacha huru.



No comments:
Post a Comment