Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, itaendelea kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa
upande wa mashtaka Juni 8 huu katika kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu
wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.
Wakili
wa Takukuru, Leonard Swai jana amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma
Shaidi kuwa kesi inayomkabili Tido leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa
kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Lakini shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo ana udhuru.
Baada
ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi
Juni 8 ili mashahidi wa upande wa mashtaka waendelee kutoa ushahidi.
Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri wamekwishatoa ushahidi .
Mashahidi
hao ni Ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC,
Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.
Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.
No comments:
Post a Comment