KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 7, 2018

BODI YA BENKI KUU YA TANZANIA (BoT) KIKAANGONI BUNGENI LEO....PAC LEO WATAWAHOJI KUHUSU MATUMIZI YA BILIONI 12

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo Alhamisi Juni 7, 2018 inakutana na bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuihoji juu ya tuhuma zinazowakabili.

Benki hiyo inatuhumiwa kutumia bima binafsi badala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

“Leo tumewaita na tutakutana nao. Baada ya kukutana nao taarifa tutaiwasilisha kwa Spika kama alivyotuagiza," amesema  mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Kaboyoka ambaye pia ni mbunge wa Same Mashariki (Chadema)

Tuhuma kuhusu BoT ziliibuliwa na mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga Juni 4, 2018 bungeni  katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango mwaka 2018/19.

Mlinga amesema BoT inatumia Sh12bilioni kwa mwaka badala ya Sh1bilioni kugharamia matibabu ya watumishi wake.

No comments:

Post a Comment