KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 14, 2018

MBUNGE AOMBA ELIMU BURE KIDATO CHA TANO NA CHA SITA

Serikali kupiti Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia, William Ole Nasha amesema lengo la serikali huko mbeleni kadiri uwezo utakavyo ruhusu itatoa elimu bure hadi chuo kikuu.

Nasha ameyabainisha hayo, leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge George Lubeleje aliyehoji “Kwa kuwa elimu bure ni kuanzia la kwanza mpaka la 12 lakini kidato cha tano na cha sita hawamo, hawa wote ni watoto wa mtu mmoja kuna sababu gani za msingi form five na Six wakaacha kusamehewa karo ? ninaomba Waziri atoe maelezo maana wote watoto ni wa kwake kwanini hao waachwe?

“Ni kweli kama alivyosema kwamba watoto wote ni watoto wa Taifa hili kwahiyo haitakiwi kuwa na ubaguzi, naomba nimuhakikishie Mh. Mbunge ni kwamba lengo la serikali huko mbele kadiri uwezo utakavyo ruhusu tutatoa elimu ikiwezekana hadi chuo kikuu bure,” amesema Nasha.

“Lakini kwasasa kutokana na hali halisi ya kifedha tutaendelea kwanza kuimarisha miundo mbinu na mazingira katika shule za ngazi ya elimu msingi kwa maana kwamba kuanzia shule za awali mpaka kidacho cha nne na kuendelea kutoa elimu bure na uwezo ukiongezeka hatuna shida ya kuongeza kidato cha tano na cha sita, lakini vilevile kama mnavyofahamu serikali inatoa mikopo kwaajili ya wanafunzi wa elimu ya juu kwahiyo anachosema ni kitu cha kweli kwahiyo uwezo ukiongezeka kidato cha tano na sita elimu bure.”

No comments:

Post a Comment