Askari
wanne wa Pori la Akiba la Mkungunero, wamefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto kwa tuhuma ya kushawishi na kuomba rushwa
ya Sh milioni tano kutoka kwa wafugaji ambao mifugo yao ilikamatwa ndani
ya pori hilo.
Akisoma
hati ya mashtaka ya watuhumiwa hao, Mwendesha mashataka wa Takukuru
Mkoa wa Manyara, Isdory Kyando mbele ya Hakimu Mkazi, Hudi Majid,
alidai tukio hilo lilitokea Mei 12 mwaka huu katika Kijiji cha
Ilkiushbouir wilayani Kiteto.
Kyando
aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Martenus Mahoka, Augustino Sadick,
Ephrahim Polepole na Godfrey Matheas wote askari wa Pori la Akiba la
Mkungunero.
Alidai
fedha hizo waliziomba kutoka kwa wenye mifugo waliokuwa wamekamatwa
ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero waweze kuiachia mifugo199 wakiwamo
ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda.
Kyando
alidai washtakiwa hao kwa pamoja wanatuhumiwa kutenda kosa kwa mujibu
wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 kifungu cha 15
(1),
Washtakiwa hao kwa pamoja walikana mashitaka na walipata dhamana hadi Septemba 17 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment