Mwanafunzi
wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Old Tanga, Shufaa Mbughuni
amekutwa amefariki dunia huku uso wake ukiwa umechubuliwa ngozi.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema mwili wa mwanafunzi
huyo umekutwa jana Agosti 19, 2018 saa 9.40 alasiri katika mtaa wa
Majani Mapana kata ya Nguvumali jijini Tanga.
Bukombe
alisema taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo ataitoa mara baada ya
madaktari wa hospitali ya mkoa wa Tanga ya Bombo kuufanyia uchunguzi
mwili wa mwanafunzi huyo.
Naye
baba wa mwanafunzi huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Majani Mapana, Salim Mbughuni amesema mwanaye aliwaaga wenzake juzi saa
2.00 usiku kwamba anakwenda kijisomea lakini hakurudi kama ilivyo
kawaida yake.
No comments:
Post a Comment