Mbunge Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina Bob Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.
Taarifa
hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali walijuzwa kuwa kesi
itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini
Kampala.
Wakati
huo huo Mtandao wa haki za binadamu za wanahabari nchini Uganda umetoa
saa 48 kwa jeshi kuwatambulisha askari wake waliowajumu wanahabari.
Kwa
upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique
Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa Mbunge Bobi wine
ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaid ya
watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani
kuachiwa.
Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wao wamekanusha.
Bob
Wine anatarijiwa kufikishwa mahakamani kwa madai ya kumiliki silaha
kinyume na sheria pamoja na tuhuma za wafuasi wake kuushambulia msafara
wa Rais Museven.
No comments:
Post a Comment