Waziri
wa Ulinzi Dk. Husein Mwinyi, amewahimiza Waislamu nchini kudumisha
amani na kuacha vitendo viovu vitakavyosababisha kutoweka kwa tunu hiyo.
Dk.
Mwinyi ameyasema hayo jana Jumatano Agosti 22, katika swala ya Eid
iliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Msife Moyo Vingunguti jijini Dar
es Salaam.
Alisema amani ndiyo tunu kubwa zaidi ambayo taifa limejaaliwa na kwamba ikitoweka hakutakuwa na nafasi ya kufanya ibada.
“Kama
mlivyosema tunu hii ndiyo kubwa zaidi, bila tunu hii hakuna nafasi ya
kufanya ibada, kwa hiyo tuache vitendo vya uvunjifu wa amanio ambavyo
matokeo yake huwaathiri zaidi wanawake na watoto,” alisema.
Aidha,
Dk. Mwinyi amelitaka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)
kuhakikisha linaleta tija kwa Waislamu wote na taifa kwa ujumla.
“Niwapongeze
kwa juhudi mbalimbali ambazo mmezifanya hasa utoaji wa huduma katika
jamii ikiwamo elimu, niwasisitize kuliombea taifa letu ambalo linapitia
changamoto nyingi pamoja na Rais wetu John Magufuli,” alisema Dk.
Mwinyi.
No comments:
Post a Comment