Na, magdalena kashindye.. Kahama
Chama
cha mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi katika uchaguzi wa marudio
katika kata ya Bugalama iliyopo katika halmashauri ya Msalala wilayani
Kahama Mkoani shinyanga.
Kwenye
uchaguzi huo uliofanyika Agosti 12 mwaka huu Vyama vitatu vilisimamisha
wagombea watatu katika kata hiyo na mgombea wa CCM Izengo Josephath
alitangazwa mshindi kwa kura 2137 akiwashinda wapinzani wake Stephano
Izengo wa CHADEMA kwa kura 571 huku mgombea wa ACT wazalendo Jilala Seni
akipata kura 32.
Uchaguzi
huo wa marudio ulifanyika kufuatia aliyekuwa diwani wa CHADEMA Izengo
Josephath kuhamia chama cha mapinduzi CCM na chama hicho kilimpa ridhaa
ya kupeperusha bendera ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment