KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 13, 2018

WALIOKUTWA NA MADINI KINYUME NA SHERIA WAHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA AU FAINI MILIONI 24

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka mitatu jela ama kulipa faini ya Sh. 24 milioni wafanyabiashara wawili wa madini baada ya kukiri kosa la kukutwa na madini ya Coloured Gemstones yenye thamani ya Dola za Kimarekani 1.8 milioni.

Pia mahakama hiyo imeamuru madini hayo yataifishwe. Hata hivyo, washtakiwa hao wameweza kuepuka kutumikia kifungo hicho baada ya kulipa faini hiyo.

Hukumu hiyo, imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande kuwasomea mashtaka mawili washtakiwa hao ambapo walikiri makosa yao.

Baada ya kukiri makosa yao, Mahakama iliradhimika kuhamia maeneo ya Msasani Kinondoni Dar es Salaam ambapo vielelezo vya kesi hiyo vilikuwepo, ambapo kesi iliendeshwa na washtakiwa kutiwa hatiani. Washitakiwa hao ni Aazam Nazim (Raia wa India) na Ango Mbossa raia wa Tanzania.

Hakimu Rwizire hivyo alimtaka kila mshtakiwa kulipa faini ya Sh. 6 milioni kwa kila kosa ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela katika kila kosa.

Kwa kuwa kila mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili hivyo kila mshtakiwa atapaswa kutoa faini ya Sh. 12 milioni iwapo atashindwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuwa vifungo hivyo vinaenda sambamba.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa yao kati ya January 2017 na June 2018 katika maeneo ya Misisiri A eneo la Mwananyamala.

Wanadaiwa kukutwa na madini aina ya Coloured Gemstones kilogramu 75,920.04 yenye thamani ya Dola za Kimarekani 1,795,687.87.

No comments:

Post a Comment