KWA mara
nyingine tena, kesi inayomkabili kiongozi wa Taasisi za Kiislamu nchini,
Sheikh Ponda Issa Ponda leo imeendelea kupigwa kalenda katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro.
Mbali na
kundi la wafuasi wa Sheikh Ponda kutoka mikoa ya Dar es Salaam na
Morogoro waliojazana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa
Morogoro leo asubuhi kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili kiongozi
wao huyo wakiwa na matumani kuwa huenda Sheikh wao angepatiwa dhamana
na kumpokea kishujaa yamekwama tena baada ya taarifa hizo.
Kesi hiyo imepigwa kalenda mpaka Januari 5, mwakani itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment