KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 26, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA INDIA.

Displaying 03.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo
Displaying 3..jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya miaka 50 ya Lions Club na Makamu wa Gavana wa Club hiyo, kwa nchi za Tanzania na Uganda, Hyderali Gangji, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda nchini India kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Displaying 6.jpg
Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Displaying 9.jpg
Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR                                                                               

No comments:

Post a Comment