Aliyekuwa kocha wa Yanga, Mbrazil
Marcio Maximo ameondoka jana kurudi nyumbani kwao Brazil na kuitakia
klabu yake ya zamani kila la kheri.
Maximo na Mbrazil mwenzake,
Leonardo Neiva wametupiwa virago na mabingwa hao wa zamani hivi karibuni
kwa kile kinachoelezwa kufanya vibaya kwa timu hiyo inayojiandaa na
michuano ya vilabu ya shirikisho la soka Afrika hapo
mwakani.‘Nawashukuru viongozi wa Yanga na mashabiki kwa muda tuliokaa
pamoja”.” Yanga ni klabu kubwa yenye malengo”.
“Nilikuwa na malengo ya kuiongoza Yanga kitaalamu zaidi, lakini inaonekana fikra zangu hazikueleweka na kuungwa mkono”.
“Tayari
kuna vilabu kadhaa vimeonesha nia ya kuniajiri lakini nitahitaji muda
kidogo kufikiria”, alisema kocha huyo aliyewahi kuifundisha timu ya
taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Maximo ameitumikia Yanga kwa
miezi mitatu na kucheza mechi tisa. Katika hizo, amefungwa mechi mbili,
moja hivi karibuni Yanga walipocheza na mahasimu wao Simba iliyochini ya
kocha Mzambia Patrick Phiri na kufungwa 2-0 katika mechi isiyo ya ligi.-BBC
No comments:
Post a Comment