Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Ukawa Profesa
Ibrahim Lipumba akiwa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na
Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbrod Slaa, alisema Kikwete anasita kumuondoa
Muhongo wakati Bunge lililishatoa maazimio ya kutaka aondolewe.
Profesa Lipumba alisema Bunge linalowakilisha
wananchi zaidi ya milioni 45 liliazimia uteuzi wa Muhongo utenguliwe
lakini rais anasema bado anachunguza.
Profesa Lipumba alisema kama Rais Kikwete
atashindwa kumwajibisha Muhongo atakuwa ameshindwa kutekeleza moja ya
maazimio ya Bunge na kwamba Ukawa litaliomba Bunge kuiwajibisha
serikali.
Alisema moja ya njia ya kuiwajibisha serikali ni pamoja na wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.
Profesa Lipumba alisema “ hivi rais anachunguza
nini haliamini bunge, kama anavyoteua mawaziri pia ana madaraka ya
kutengua nafasi zao, sasa anasita nini wakati ni azimio la bunge
limemwelekeza, ikumbukwe kuwa bunge kwa niaba ya wananchi ndilo lenye
jukumu la kuisimamia serikali,” alisema Lipumba.-MWANANCHI
No comments:
Post a Comment