KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

February 26, 2015

UKAWA WANATAKA DAFTARI LA WAPIGA KURA LIBORESHWE, KATIBA MPYA ISUBIRI


Fredy Azzah, Dar es Salaam UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umedai kubaini mpango wa siri wa Serikali kutaka kuipitisha kwa hila Katiba Inayopendekezwa itumike kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu.Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe, alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Wananchi (CUF) Buguruni, Dar es Salaam.“Tumepata taarifa kuwa CCM imeamua aidha inyeshe mvua au isinyeshe, Katiba Inayopendekezwa itapita kwenye kura ya maoni waweze kuutumia kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.“Tunamuomba Rais Kikwete amalize muda wake wa miaka 10, aondoke atuachie nchi yetu ikiwa salama kwa sababu mbinu hizo zinazoandaliwa zinahatarisha amani ya nchi,” alisema Mbowe.Alisema wamepata taarifa kwamba baadhi ya sheria zimeanza kufanyiwa marekebisho lengo likiwa ni kuhakikisha Katiba hiyo inapita na kutumika kwenye uchaguzi mkuu ujao.Akitoa mfano, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekuwa ikitumiwa kutoa matamko ambayo wakati mwingine hayana ukweli wowote.“NEC wanasema siyo lazima kupitia na kuhakiki Daftari la Kudumu la Wapiga kura baada ya kuandikishwa, suala hili siyo uamuzi wao ni sheria inayowataka lipitiwe baada ya kuandikwa,” alisema Mbowe. MTANZANIA

No comments:

Post a Comment