Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast anayekipiga Liverpool, Kolo Toure amesema kuwa ataondoka Liverpool kama hatakuwa akipewa nafasi katika kikosi cha klabu hiyo.
Toure ambaye ameshawahi kuchezea Arsenal na Manchester City kwa upande wa kocha wa Liverpool, Judgen Klopp ameshaonekana kuhitaji kuendelea kuwa na mchezaji huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni kwa msmu huu.
“Ni jambo zuri kusikia hivyo kutoka kwa meneja mkubwa (kumbakisha Liverpool),
“Lakini kama nikipata nafasi kwenye kikosi, nitakuwa na furaha zaidi lakini kama sitapata haitakuwa na jinsi,” Toure aliwambia BBC Sport.