Jumla ya wagonjwa 267 wa mkoani Njombe
wamenufaika na huduma za matibabu za madaktari bingwa kutoka hospitali
mbalimbali za hapa nchini.
Takwimu hizo zimetolewa leo mkoani Njombe na
Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu
wakati akitoa taarifa za maendeleo ya zoezi la utoaji wa huduma za afya
kwa wananchi chini ya ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Amesema kuwa kati ya wagonjwa hao, 13
wamepatiwa huduma ya upasuaji kutoka kwa madaktari bingwa pia huduma
hizo zinaendelea kutolewa katika Hospitali ya Kibena mkoani humo.
“Tunawashukuru sana wananchi wa Mkoa wa
Njombe kwa kuitikia wito wetu, leo ni siku ya tatu lakini tumeshawapatia
matibabu jumla ya wananchi 267 kati ya hao wagonjwa 13 wamepatiwa
huduma ya upasuaji, tunawasihi waendelee kuja kwakua bado tuna siku
mbili za kuendelea kuwapatia huduma za afya”alisema Singu.
Amefafanua kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa
waliopatiwa matibabu mkoani hapo ni wanawake ambao wengi wao
wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo pamoja na mfumo wa mkojo.
Lengo wa mpango huu wa kutumia madaktari
bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Rufaa za
Kanda ni kuhakikisha kuwa huduma za matibabu kutoka kwa madaktari
bingwa zinawafikia wanachama wa Mfuko huo na Watanzania kwa ujumla
popote walipo.
Mpaka sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
umepeleka huduma ya madaktari bingwa katika Mikoa 14 ikiwa na lengo la
kuhakikisha huduma bora za matibabu zinatolewa kwa usawa.
Singu ametoa wito kwa wananchi wa mkoani
Njombe kuendelea kujitokeza kwa wingi kujipatia matibabu kwa kuwa huduma
hizo zinatolewa kwa gharama nafuu.
|
April 27, 2016
WAKAZI 267 WA MKOANI NJOMBE WANUFAIKA NA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment