Mfanyabiashara raia wa China aliyetambulika kwa jina la Luo Dongpeng (32), maiti yake imekutwa ndani ya gari lenye namba za usajili T145 DFY Machi 28, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar,Uwazi linakupasha.
Waliendelea kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma, walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama.
Moja ya msumali uliokuwa umetegwa kwenye gari hilo.
Mashuhuda hao walidai kuwa huenda Mchinia huyo aliuawa kisha
kutelekezwa na gari lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi
na shingoni.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment