Kampuni ya Safari Indoor Digital
pamoja na kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express leo hii wamezindua
rasmi huduma ya kisasa ya kutoa elimu mbalimbali kwa abiria kupitia TV
(Screen) za kwenye mabasi.
Hayo yamesemwa na Meneja
operesheni wa kampuni ya Safari Indoor Digital Bi.Doreen Minja alipokuwa
akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo
jijini Dar es Salaam.
Bi Doreen amesema kuwa katika
programu hiyo kampuni yao ya safari indoor digital watatumia screen za
ndani ya mabasi ya kampuni ya Kilimanjaro express na jitihada mbalimbali
zinafanyika ili huduma hii kufika katika mabasi yote.
Aidha huduma hiyo itasaidia
kumpatia abiria habari mbalimbali anapokuwa safarini kama haki yake ya
msingi katika Nyanja za kijamii,kiuchumi na elimu na hasa elimu ya
afya,sheria na biashara uku ikimwezesha abiria kutambua mambo mbalimbali
ndani ya nchi na nje.
Hata hivyo kampuni ya Safari
Indoor Digital watakuwa na kipengele cha matangazo kwa kanda ambacho
kitasaidia abiria kuweza kutambua fursa mbalimbali za mkoa uendao na
hata kujua viongozi wa mkoa husika na watashirikiana na jeshi la POLISI
na SUMATRA na chama cha kutetea abiria Tanzania (CHAKUA) kwa ujumla
kutoa elimu katika screen hizo kuhusu haki mbalimbali za abiria,sheria
za usalama barabarani kwa kutengeneza kipindi maalum kitakachoelimisha
jamii kuhusu suala hilo.
Nao chama cha kutetea abiria
Tanzania (CHAKUA) kimewaasa abiria wote nchini kuitumia fursa hii vizuri
kwani itawasogezea huduma za muhimu karibu kwani hata namba za simu za
Polisi,Sumatra na Chakua zitapatikana katika screen hizo pindi
linapotokea tatizo safarini.
|
June 3, 2016
KAMPUNI YA SAFARI INDOOR DIGITAL (SID) KUTOA ELIMU KUPITIA MABASI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment