Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania Bi. Melisa John (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda nchini Nigeria kushiriki michuano ya shindano hilo kwa nchi za Afrika,wa pili kushoto ni Meneja Mahusiano Airtel Bw.Jackson Mmbando. |
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa
kumuaga mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Bi.
Melisa John (kulia) anayetarajia kushiriki mashindano hayo nchini Nigeria Juni 11mwaka huu litakaloshirikisha nchi za tisa za Afrika (kushoto) Meneja Mahusiano Airtel Jackson Mmbando . |
Meneja Mahusiano Airtel Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya Airtel ya kuwawezesha Vijana katika sanaa ya muziki leo Jijini Dar es Salaam,(katikati) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi na (kulia) mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Bi. Melisa John. |
Mshindi
wa Shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Bi. Melisa John
(kulia) akiimba moja ya nyimbo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar
es Salaam (hawapo picha) alipokuwa akiagwa na kukabidhiwa bendera ya
Taifa kwa ajili ya kuwakilisha nchi katika mashindano yanayotarajiwa
kufanyika nchini Nigeria Juni 11 mwaka huu, (katikati) Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Bi.Leah Kihimbi na (kushoto) Meneja Mahusiano Airtel Jackson
Mmbando akifurahia wimbo huo.( Picha na Anitha Jonas).
Na Lorietha Laurence
Taasisi
na Mashirika binafsi nchini zimeombwa kushirikiana na serikali katika
kutekeleza sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayosisitiza
kukuza na kuendeleza sanaa na wasanii kwa lengo la kuinua vipaji na
kutimiza ndoto za vijana wengi wanajihusisha na sanaa.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi wakati wa
kukabidhi bendera ya Taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Star Bi.
Melisa John ambaye ataiwakilisha nchi katika mashindano ya Airtel Afrika
nchini Nigeria.
Bi.Kihimbi
ameleeza kuwa fursa inayotolewa na Kampuni ya Airtel ni adhimu na mfano
tosha kwa makampuni, taasisi na mashiriki mengine nchini kuunga mkono
juhudi hizo kwa kuanzisha program za kuwakwamua vijana kiuchumi kupitia
sanaa ya muziki.
“Sanaa
ya muziki ni kazi kama kazi nyingine,hivyo nashukuru kampuni ya Airtel
kwa kuamua kuunga mkono serikali katika mpango huu wa kuibua vipaji vya
vijana kupitia sanaa ya muziki” alisema Bi.Kihimbi.
Aidha
aliongeza kuwa nafasi aliyoipata Melisa ni adhimu hivyo haina budi
kutumia fursa hiyo vizuri kwa kuikuza talanta yake ya kuimba na
hatimaye kukua kimuziki na kuweza kuitangaza nchini kitaifa na
kimataifa.
Naye
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema kuwa kampuni yao ipo
tayari kuendelea kuwekeza katika sanaa kwa kuwawezesha vijana pamoja na
wanamuziki chipukizi kuweza kufikia ndoto zao kupitia Airtel Trace Music
Star.
“Tunafurahi
kuwawezesha wanamuziki chipukizi vijana kupata nafasi adimu za kufanya
kazi na magwiji wa muziki duniani kama Akon na Keri Hilson hivyo
tunaomba watanzania watumie fursa
hii kwa kushiriki katika mashindano ya Airtel Trace Music Star ili waweze kukuza vipaji vyao”alisema Bw. Mmbando.
Kwa
upande wake mshindi wa Airtel Trace Music Star Bi.Melisa John
ameishukuru Serikali na Airtel kwa ushirikiano wao katika kukuza tasnia
ya muziki na kuchochea ajira kwa vijana
wengi na kuahidi kurudi na ushindi.
Shindano la Airtel Trace Music Star Kitaifa
yalifanyika jijini Dar es Salaam ambapo Bi.Melisa John aliibuka mshindi
na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo kimataifa
yatakayoshirikisha nchi tisa ambazo ni
Niger,DRCongo,Gabon,Malawi,Nigeria,Madagascar,Kenya,Zambia na Ghana
yanayotarajiwa kufanyika nchini Nigeria Juni 11 mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment