Pokea picha ya Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Katibu Mkuu wa Shirakawa La Mawasiliano la Jumuiya ya Madola, Eng. Shola Taylor wakati alipokutana naye mjini Daodoma leo. |
Katibu Mkuu wa Shirakawa La
Mawasiliano la Jumuiya ya Madola, Eng. Shola Taylor akitoa ufafanuzi
baadhi ya mambo wakati alipokutana na Pokea picha ya Prof. Makame
Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mjini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………………
Pokea picha ya Prof. Makame
Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Katibu Mkuu wa
Shirika La Mawasiliano la Jumuiya ya Madola, Eng. Shola Taylor akiwa
na mazungumzo nae ofisini kwake, Dodoma kuhusu kuipatia Tanzania msaada
wa kiufundi wa kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao
yaani the National Cybersecurity Strategy na the National Broadband
Strategy.
Tanzania imekidhi vigezo vya kupatiwa msaada huo kwa kuwa
tayari nchi ina sera, sheria, kanuni inayosimamia na kuendeleza Sekta
ya TEHAMA nchini. Nyaraka hizo ni pamoja na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya
mwaka 2016, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Pia uwepo wa
miundombinu mbalimbali ya TEHAMA kama vile Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano na Kituo Mahiri cha Kutunzia Data.Wadau mbalimbali zaidi ya 60 wa kutoa Taasisi za Serikali, Sekta binafsi na mashirika yasiyokuwa ya Serikali wamekutana kwa pamoja na kujadiliana namna ya kuandaa Mkakati wa Taifa wa Usalama kwenye Mtandao. Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam kuanzia tare he 31 Mei, 2016 na kumalizika tarehe 3 Juni, 2016. Aidha, Tanzania ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola ambapo ni mwanachama hai anaestahili kupatiwa msaada huo kutoka Jumuiya hiyo. Nchi nyingine za Afrika ambapo zinaandaa Mkakati huo ni pamoja na Botswana, Rwanda na Malawi na nchi ambazo tayari zina Mkakati huo ni Uganda. |
No comments:
Post a Comment