Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi Akisoma hotuba ya uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Zambi alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Lindi ikiwa ni mmoja wapo. |
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi pamoja na washiriki toka katika Halmashauri 6 za Mkoa Huo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi(Mwenye suti ya bluu katikati waliokaa)Mara baada ya Uzinduzi wa Mradi huo Mjini Lindi |
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria Ofisi ya Rais TAMISEMI,Edwin Mgendera alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma |
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi pamoja na washiriki wengine wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo |
Kutoka Kushoto Ni Mkuu wa Wilaya
ya Ruangwa,Mariam Mtima,Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,Pololeti Mgema na
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Ephraim Mbaga Wakifuatilia kwa Umakini Hotuba
ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati wa Ufunguzi huo.Picha na Habari kwa Hisani ya Abdulaziz Video-Lindi
………………………………………………………………………………………………………..
Katika kuimarisha Ubora wa Utoaji
huduma za Umma na Matumizi yake kwa ajili ya Kuboresha na kuimarisha
Mifumo,Mkoa wa Lindi Umezindua Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya sekta za
umma utakaowezesha Jamii katika Ngazi ya halmashauri kutumia rasilimali
kwa Uwazi na kuwezesha ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na
kufuatilia matokeo ya kila sekta
Mpango huo utakaosaidia utoaji wa
ushauri wa kitaalamu na kuwajengea uwezo wafanyakazi ili kuongeza
Usawa wa mgawanyo wa rasilimali watub kwa ajili ya utoaji bora wa huduma
katika maeneo yenye Uhitaji zaidi ikiwemo mfumo wa ajira pamoja na
kudumisha watumishi katika Ajira Serikalini
Akizindua Mradi huo wa PS 3,Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amesema kuwa mradi huo wa uhimarishwaji
wa mifumo ya sekta za Umma nchini utasaidia kuondoa tatizo sugu la
watumishi hewa endapo utekelezaji wake utafanyika vizuri.
Awali akitoa taarifa katika
uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mradi katika Mikoa, Dk.Conrad Mbuya alisema
mradi huo utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri
inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza
ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.
Kufuatia Uzinduzi wa Mradi
huo,Mkuu wa Wilaya ya Lindi Yahya Nawanda pamoja na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Abuu MjakA walieleza kuwa mradi huo pia
utasaidia ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma ikiwemo
ushirikishwaji wa Madiwani katika Utekelezaji wa mradi huo Utakaoboresha
Utendaji na Uwajibikaji katika kutoa huduma kwa Jamii
Mradi huo uliozinduliwa leo
unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara ambayo ni Iringa, Dodoma,
Kagera, Kigoma,Mara,Mbeya, Morogoro, Mtwara,Mwanza, Njombe, Rukwa na
Shinyanga pamoja na Lindi.
|
No comments:
Post a Comment