Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Klabu ya Yanga, Salvatory Edward (kushoto) akisaidia kupima eneo atakalokabidhiwa mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga.Kulia ni Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib. |
Mwenyekiti
wa SHIWATA, Cassim Taalib wa pili kulia akisoma ramani ya eneo la
kukabidhiwa mchezaji bora Afrika, Mbwana Samatta wakati wa kupima eneo
hilo atakalokabidhiwa jumapili. Kulia ni mchezaji wa zamani ya Stars na
YAnga, Salvatory Edward na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa SHIWATA,
Mohamed Kisoky.
………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
SHEREHE za kukabidhi kiwanja cha ekari tano kwa mchezaji bora
barani Afrika, Mbwana Ali Samatta unafanyika Jumapili 5,2016 kwenye
kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib alisema jana jijini Dar es SAlaam kuwa maandalizi yamekamilika na Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya TAifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi. Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha ya wanachama 180 waliokwisha kabidhiwa nyumba zao. Alisema SHIWATA imemzawadia Mbwana ekari tano ili ajenge kituo cha michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania watakaolitangaza taifa hili kwenye medani ya michezo kimataifa. Taalib alisema mtandao huo unaomiliki eneo la ekari 300 za kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji. Alisema sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185 wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana. Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa HAbari, Utamaduni na Sanaa, NApe Mnauye ambaye atakuwa waziri wa pili kutembelea kijiji hicho baada ya NAibu WAziri wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka huu. Viongozi wengine waliowahi kutembelea kijiji hicho ni kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2014, Wakuu wa wilaya ya Mkuranga wastaafu, Mercy Silla, Clemency na Mkuu wa wilaya hiyo wa sasa, Abdallah Kihato.
Wageni wengine walioalikwa kwenye
sherehe hizo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ITFF),
Jamal Malinzi viongozi wa Serikali wa Wilaya ya Mkuranga na wasanii
maarufu nchini.
|
No comments:
Post a Comment