Benjamin Sawe-Maelezo-Dar es Salaam
MTAFITI wa uchumi katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Haji Semboja aimepongeza hatua ya
Serikali ya kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier- 8 Q400 na
kusema zitasaidia kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini na
kuchangia katika ukuaji wa uchumi.
Prof. Semboja aliyasema hayo leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano maalum na MAELEZO kuhusu
mikakati na hatua ya Serikali ya kulifufua upya shirika la ndege nchini
(ATCL).
Profesa Semboja alipingana na
maoni ya baadhi ya watu wanaokosoa kasi ya ndege hizo, kwani kulingana
ndege hizo zimekidhi mahitaji ya usafiri wa abiria wa ndani na nje ya
nchi ikilinganishwa na ndege nyingine za aina yake kama ATR
Akizungumzia kuhusu kupanda kwa
gharama za matengenezo na uendeshaji wa baadhi ya ndege nyingine nchini,
ikiwemo mahitaji ya ongezeko la mishahara kwa marubani, Profesa Semboja
alisema kuna uwezekano mkubwa kwa Bombardier- 8 Q400 kuendeshwa kwa bei
rahisi na ikauza tiketi zake kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege
nyingine.
“Shirika letu la ndege lilikuwa
na hali mbaya kutokana na kushindwa kujiendesha kutokana na gharama
kubwa za uendeshaji na abiria wachache, wanaotumia usafiri wa
anga”.Alisema Profesa Joseph Semboja
Alisema ndege hizo zitaimarisha
mtandao wa huduma za usafiri wa anga kwa soko la ndani, lakini pia
zitaongeza ushindani na kuleta unafuu wa bei kwa watumiaji wa usafiri wa
anga,
“Zitaimarisha sekta za biashara
na uwekezaji na kuwezesha watalii kutembelea vivutio vya ndani ya nchi”
Alisema Profesa Joseph Semboja.
Aidha Prof. Semboja aliwataka
Watanzania wote wakiwemo wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi
kusafiri kwa kutumia ndege hizo ili Kampuni ya ATCL ijiimarishe na iweze
kujiendesha kibiashara baada ya kutegemea bajeti ya Serikali
No comments:
Post a Comment