KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 29, 2016

UTAFITI TWAWEZA: ASILIMIA 89 YA WATANZANIA WALIOHOJIWA WASEMA HAKUNA UDIKTETA NCHINI

Ripoti ya Twaweza, Septemba 29, 2016.

#Wananchi 1,602 wamehojiwa kati ya Agosti 24 na 29 kwa njia ya simu maeneo mbalimbali nchini kuhusu demokrasia, udikteta na maandamano

#Demokrasia: asilimia 80 ya wananchi wanasema baada ya uchaguzi wanataka maendeleo na sio siasa.

#Watanzania wengi wanaunga mkono demokrasia kuwa mfumo mzuri wa kisiasa lakini wengi hawadhani kama Tanzania inaongozwa kidikteta.Wanaoamini kuna udikteta Tanzania ni 11% tu.

#Ni wananchi watatu tu kati ya 10 wanaounga mkono maandamano

#Zaidi ya nusu ya wananchi (sita kati ya 10) wanaunga mkono kuzuiwa mikutano isiyo na tija ambapo mmoja kati ya watatu wanaojitambulisha kuwa wafuasi wa upinzani pia akiunga mkono zuio hilo.

#wananchi wengi wasio na vyama wanaunga mkono zuio la mikutano holela ya kisiasa (53%); 

#Ni mwananchi mmoja tu kati ya sita (sawa na asilimia 16 tu) anayejua Ukawa hasa inasimamia nini huku zaidi ya asilimia 70 hawajui umoja huo unasimamia nini hasa

#Ni wananchi wachache sana (1 kati ya watano sawa na 22%) wanaounga mkono Ukawa huku asilimia 44 ya wanachama waliojitambulisha kuwa wa Ukawa wakiwa hawaungi mkono mwenendo wa umoja huo.

#Wananchi wengi (9 katika 10 sawa na asilimia 85) wasingeshiriki maandamano ya Ukawa Septemba mosi ambapo kati ya hao ni asilimia 24 tu ya wafuasi wa umoja huo ndio wamesema wangeshiriki.

#Wananchi wengi wanaamini upo uhuru wa kujieleza na wanaona wako huru kukisoa Serikali.

No comments:

Post a Comment