Na Mwamvua Mwinyi
WAZIRI
mkuu ,Kassim Majaliwa ,amewataka wafugaji hususan wamang’ati,wamasai na
barbeig nchini kufuga kisasa na kuachana na ufugaji wa kuzurura na
mifugo bila manufaa .
Aidha
amesema wafugaji hao wanapaswa kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa kuuza
mifugo yao kwa tija badala ya kuona ufahari wa kukaa na kundi kubwa la
mifugo.
Akizungumza
na wananchi wilayani Kibiti,alieleza kuwa wafugaji wanatakiwa kuelimika
kuhusiana na suala hilo ili kupunguza ama kuondoa tatizo la migogoro
ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengi hapa nchini.
Majaliwa
amewaasa wafugaji waridhie kuuza mifugo yao minadani wasikae nayo na
kuhamahama nayo kiholela bila mpangilio kwenye vijiji na wilaya zisizo
na maeneo kwa ajili ya mifugo.
Ameongeza
kuwa kuna kila sababu ya kuwashauri wauze baadhi ya Ng’ombe wao na
kubaki na Ng’ombe wachache kuliko kukaa na kundi kubwa.
“Wafugaji
ridhieni kuwauza Ng’ombe,Mbuzi,Kondoo zenu ,msikae nao kuzurula nao
misituni,uzeni mbakie na mifugo mtakayoimudu pasipo kusababisha
changamoto kwenye jamii”
“Ndio
maana serikali inasisitiza viwanda ,na tunakaribisha wajenzi wa ndani
na nje ya nchi ,waje wajenge viwanda vingi ikiwemo vya kusaga nyama za
ng’ombe ,kondoo ili ng’ombe hawa waishie viwandani”
Hata hivyo ameeleza kuwa serikali
imewakataza wafugaji wote kuwa ni marufuku kupeleka mifugo kwenye
mazao ya wakulima ili kuondokanana tatizo kubwa la migogoro baina ya
wakulima na wafugaji.
Majaliwa ametoa rai kwa wafugaji waridhie mpango wa serikali wa matumizi bora ya ardhi .
Amesema haiwezekani ng’ombe
atembee hapa hadi Morogoro hata akichinjwa itakuwa sio nyama nzuri hivyo
amewaomba waondokane na kasumba ya kutembeza ng’ombe umbali mrefu kwani
ni ufugaji usio na tija.
No comments:
Post a Comment