![]() |
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na Wanahabari leo, Makao Makuu ya chama hicho Jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
ametangaza kufutwa kwa maandamano na mikutano ya kupinga Udikteta nchini
maarufu kama Ukuta na badala yake amesema watatumia mbinu nyingine mpya kuibana
serikali.
Amesema walikubalina kuwapa muda
viongozi wa dini ili wandeshe majadiliano na serikali yenye lengo la kufikia
muafaka lakini hadi sasa anasema hakuna kilichofanyika
“Jana tulikutana tena kupata
mrejesho wa swala hilo,taarifa ambayo Kamati Kuu imepewa ni kwamba vingozi wa
dini hawakujanya lolote,”.
Ameongeza kusema kuwa wao kama chama
cha siasa wanawaheshimu viongozi wa dini na kwamba kwa sasa wataendelea na harakati zao za kudai haki kwa kutumia mbinu nyingine.
“Baada ya kuona mambo kadhaa
yalitopo tumeamua kusitisha maandamano ya Oktoba Mosi ili kupisha mbinu nyingine mpya” alisema
Amefanua kuwa tukio la kudai haki
sio tukio la siku moja kama wengi wanavyodhani na kwamba mbinu mpya ni
kuyashawishi mataifa ya Ulaya yaibane serikali.
“Chama kilituma Ujumbe maalum Ulaya
kuielezea Jamii ya kimataifa ukandamizaji unaoendelea nchini na kwamba misafara
mingine ya chama itaendelea kwenda nchi nyingi zaidi kufanya mikutano na Jumuiya
ya kimataifa na kuifahamisha kwamba Tanzania ile ya amani haipo tena,” alisema
Pia alisema wanaendelea na
maandalizi ya kufungua kesi mbalimbali kuhusu yanayoendelea nchini.CHANZO HABARI24
|
September 30, 2016
MBOWE ATANGAZA KUFUTA MAANDAMANO NA MIKUTANO YA UKUTA KESHO, ASEMA WATATUMIA MBINU NYINGINE KUDAI HAKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment