Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba leo ametamba kuwa
yeye ni mwenyekiti halali wa chama hicho na kwamba hakuna mtu yeyote
atakaye mvua wadhifa huo zaidi ya maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu
ambao amedai kuwa asilimia kubwa wana muunga mkono.
Lipumba ameyasema hayo katika ofisi za makao makuu ya CUF yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
Lipumba
amesema kuwa yeye bado ni mwenyekiti halali wa CUF Taifa kwa kuwa
aliitengua barua ya kujiudhuru kwake kabla ya mkutano mkuu wenye mamlaka
ya kukubali barua ya kujidhuru kwake kuketi na kuiridhia.
Pia
amesema kikao kilichoketi Zanzibar cha Baraza Kuu la Uongozi CUF
kilikuwa batili kwa kuwa hakikufuata utaratibu na kanuni za katiba ya
chama hicho. Amefafanua kwamba , katiba ya CUF inasema kuwa mwenye
mamlaka ya kuitisha mkutano au kikao cha dharula ni Katibu Mkuu wa Chama
hicho na kwamba Maalim Seif Shariff Hamadi mwenye wadhifa huo alikuwa
nje ya nchi, hivyo aliyekuwa na mamlaka ya kukaimu wadhifu huo ni Naibu
Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya ambaye hakupewa taarifa ya kikao
hicho na wala hakuitisha kikao cha kamati ya utendaji ambacho
kingeidhinisha kufanyika mkutano huo, na wala hakuitisha mkutano huo.
Hata
hivyo, Profesa Lipumba amesema katiba ya CUF inasema kuwa mwenyekiti
huvuliwa wadhifa wake pale ambapo wajumbe wa mkutano mkuu kutoka Bara na
Zanzibar kuridhia kuvuliwa uenyekiti na kwamba hayo hayakufanyika.
“Ukizingatia
katiba usingepata theluthi mbili ya wajumbe wa mkutano mkuu ambao
wangeikubali barua ya kujiudhuru kwangu, ” amesema.
Katika hatua nyingine Lipumba amesema anatarajia kuteua wakurugenzi wapya siku za hivi karibuni.
“Mamlaka niliyonayo yananiruhusu kuteua wakurugenzi, na hiyo kazi nitaifanya nitakapo imaliza nitawajulisha,” amesema.
Hali
kadhalika, Lipumba amesema wabunge, viongozi na wanachama waliovuliwa
na au kusimamishwa uanachama watarejea kwenye wadhifa wao kwa kuwa
maamuzi ya kusimamishwa na au kufukuzwa kwao yalikuwa batili.
Amemtaka
Katibu Mkuu Maalim Seif kushirikiana nae na kumtoa wasisi kuwa akifika
katika ofisi hizo hatodhulika na walinzi wa chama hicho kwa kuwa wako
kikatiba kulinda mali na viongozi wa chama hicho.
“Asiwe
na wasiwasi kwa ajili ya walinzi kwa sababu wako kikatiba, mimi wala
sijaenda omba ulinzi polisi na sijawaona hapa, waliokuwepo ni walinzi wa
kila siku na anawafahamu, ” amesema.
Ameongeza kuwa “Katibu mkuu afuate katiba yetu, na kwenye siasa watu hutumia hekima kwa sababu mawazo tunatofautiana,”
Kuhusu
mgogoro uliokuwepo CUF, amesema atawasilina na Baraza la Wazee waasisi
wa CUF ili wamsihi Maalim Seif akubali suluhu ya mgogoro huo.
Amesema
CUF itaendelea kuwa imara na haitameguka kama baadhi ya watu
wanavyosema na kuwaomba wanzanzibar kutokubali kurubuniwa na kudanganywa
kuwa yeye hana uchungu na taifa hilo.
“Matatizo
ya Zanzibar yanajulikana yapo kwa muda mrefu, miaka mingi nimekuwa
nikitetea masilahi ya wanzanzibar hata siku moja sikuona viongozi wa
Chadema wakiwatetea zaidi ya marehemu Bob Chacha Wangwe,” amesema.
No comments:
Post a Comment