![]() | ||
Waandishi wa habari, wakimsikiliza Mwenyekiti wa CUF Profesa Lipumba Ofisi za MaLipumba anaongea na wanahabari Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba leo amezungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni na kusema kuwa hana taarifa yoyote ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Hamad katika Ofisi za chama hicho leo na kusema kuwa hana pingamizi na jambo hilo kwani hizo ni Ofisi za Maalim Seif pia. Amesema iwapo Maalim Seif atawasili ofisini hapo basi atamkabidhi majukumu na miongozo ya chama hicho . kuhusu uwepo wa Polisi eneo hilo la Ofisi alisema "Hatujaita polisi waje wafanye doria kama wapo sina taarifa nao". Amesema kwamba anastaajabu kusikia Maalim Seif anaenda kuomba ulinzi wakati ana walinzi wa serikali na walinzi wa chama na kwamba hakuna haja ya kwenda kuomba ulinzi wa Polisi. "Sijazungumza na Seif ila namueleza kuwa Mimi ni mwenyekiti wa Taifa na yeye ni Katibu Mkuu tulichaguliwa siku moja asiwe na wasiwasi aje ofisini kwake" alisema. Awali kulikuwa na taarifa kwamba Maalim angekwenda Ofisini hapo leo asubuhi lakini angeenda kwanza kuomba ulinzi. Kwa mujibu wa katiba mwenyekiti wa chama anafukuzwa na mkutano mkuu wa chama na sio vikao vya Facebook.Mimi ni mwenyekiti. Chadema ndio mabingwa wa kuleta fitna huku kwetu.cuf ipo imara Lipumba kamaliza |
September 30, 2016
PROFESA LIPUMBA ALONGA LEO, ASEMA ANAMSUBIRI KATIBU WAKE AENDE KUMPA MAJUKUMU YA KAZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment