Naibu
waziri ofisi ya Rais Tamisemi kushoto Seleman Jafo akipena mikono na
Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wilaya ya
Kisarawe,(UWAMAMI) baada ya hafla fupi ya kukabidhiana madawati 150
yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 15.
Naibu
waziri ofisi ya Rais Tamisemi akizungumza na watendaji wa halmashauri
ya wilaya ya Kisarawe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 150 kwa
ajili ya kuwasaidia wanafunzi kuondokana na tatizo la kukaa chini (PICHA
ZOTE NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE.
NAIBU
waziri ofisi ya rais Tamisemi Selaman Jafo amewaagiza maafisa elimu wa
shule za sekondari na msingi hapa nchini kuachana na tabia ya kufanya
kazi kwa mazoea ya kushinda wakiwa wamekaa ofisini tu bila ya
kujishughulisha na badala yake wanapaswa kuhakikisha wanakwenda katika
maeneo ya kazi hususan ya vijijini kwa ajili ya kuweza kubaini
changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa
madawati, vyoo pamoja na madarasa.
Jafo
ametoa agizo hilo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 150 kwa
niaba ya serikali katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa
Pwani yaliyotolewa na umoja wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu
(UWAMAMI) iliyofanyika wilayani humo.
Alisema
kwamba kuna baadhi ya maafisa elimu hawatambua majukumu yao ipasavyo
hivyo kutokana na agizo lililotolewa na Rais Dr. John Magufuli la
wanafunzi wote kusoma wakiwa wamekaa chini ya madawati atahahakikisha
anawavalia njunga watendaji wote watakaobainika wanakwamisha kwa
makusudi juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
“Kwa
kweli kuna baadhi ya maafisa elimu wengine wana tabia ya kukaa tu
mezani hawaendi kujishughulisha na kuangalia changamoto za vijijini, ili
kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya
elimu hapa nchini kwa hiyo ninawaomba sana tucahpe kazi kwa bidii, ili
tuweze kuleta maendeleo ya elimu,”alisema Jafo.
Aidha
Jafo baada ya kukabidhiwa msaada huo wa madawati amebainisha kuwa
licha ya utekelezaji wa agizo la rais la utengenezaji wa madawati kwa
halmashauri zote nchini kufikia kiwango cha asilimia 98 hadi sasa,
lakini bado kuna changamoto nyingine ya uhaba ma madarasa,matundu ya
vyoo pamoja na nyumba za kuishi walimu.
No comments:
Post a Comment