Bohari ya Dawa (MSD) hii leo
imekabidhiwa mashine za kupandishia mizigo juu na kushusha (Forklifts)
sita, zenye gharama ya shilingi za Kitanzania Milion 531. 8, ambazo
zimetolewa msaada na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund kupitia Shirika
la Marekani la Ushirikiano wa Kimataifa (USAID).
Msaada huo ni sehemu ya awamu
ya pili ya maboresho ya maeneo ya kuhifadhia dawa ya MSD ualiyokuwa
yakifanywa na Global Fund, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa maghala ya
kisasa yaani WiB ya MSD Makao makuu, Dodoma naMbeya, na ujenzi wa
maghala ya Kisasa MSD kanda yaTabora na Kituo cha mauzo Tanga.
Wakizungumza katika
makabidhiano hayo, katika utekelezaji wa awamu ya mwisho ya upanuzi na
ujenzi wa maghala ya kisasa yanayojulikana kama Warehouse in -a –box,
mashinehizo (forklifts), Naibu Mkurugenzi Mkazi wa JSI/SCMS Marasi
Mwencha amesema fedha hizo ni zilezilizosalia kutoka kwenye ujenzi wa
maghala ya kisasa ya MSD, ambapo walikubaliana na menejimenti ya MSD
kununulia forklift.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amewashukuru wa hisani hao kwa
mashine hizo ambazo ni za gharama, na kueleza kuwa mashine hizo
zitapelekwa kwenye kanda za MSD zenye uhitaji. Hata hivyo ameeleza kuwat
ayari MSD ina Kiwanja maeneo ya Luguruni, wilayani Ubungo jijini
DSM,kwa ajili ya kujenga ofisi na ghala la kisasa kwa Kanda ya DSM hivyo
wanategemea kuendelea kushirikiana na wa hisani kwa ajili ya ujenzi
pindi taratibu zitakapokamilika.
|
February 14, 2017
MSD YAPATA FORKLIFT SITA KUTOKA GLOBAL FUND
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment