Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) leo Februari 07, 2017 jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau kuhusu mambo mbalimbali katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. |
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 07,2017 jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau kuhusu mambo mbalimbali katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. |
Waandishi wa Habari wakifuatilia
mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akizungumza na waandishi wa
habari leo Februari 07,2017 jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara
kuanza kuzungumza na wadau kuhusu mambo mbalimbali katika sekta
zinazosimamiwa na Wizara yake.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
…………………………………………………………………………..
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Tarehe: 07/02/2017
Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya kushirikisha wadau
inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata vionjo, maoni,
mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya kama
wadau wake wanavyotegemea.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
alipokua akizungumza na waandishi wa habari kutangaza programu hiyo
yenye kauli mbiu ya kuitoa wizara ofisini kuipeleka kwa wadau leo Jijini
Dar es Salaam.
Prof. Gabriel amesema kuwa Wizara
imekua na kauli mbiu ya kuitoa Wizara Dar es Salaam kuipeleka mikoani
na sasa inaendelea na mkakati wa kuitoa wizara ofisini na kuipeleka kwa
wadau kwani Shabaa kubwa ya wizara ni kuhakikisha kwamba yale
yanayofanywa na wizara jamii iyafahamu katika kutekeleza nia na hari ya
hapa kazi tuu ya serikali ya awamu ya tano.
“Mpango wa programu ya wadau
tuzungumze utafanyika kisekta ambapo utakua ni mkutano utakaoshirikisha
mmoja wa viongozi wa wizara kukutanana na wadau na utakua na utaratibu
madhubuti kwa kila mwezi siku ya jumanne saa nne asubuhi ambapo viongozi
hao watakutana na vyombo vya habari wakiwa na wadau kujadili mambo ya
kisekta” amesema Prof. Gabriel
Mpango huu utahusisha Jumanne ya
kwanza ya mwezi sekta ya habari na wadau wote wa habari, jumanne ya pili
ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya Utamaduni na wadau wote wa utamaduni,
jumanne ya tatu ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya sanaa na wadau wote
wa sanaa na mwisho jumanne ya nne ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya
maendeleo ya michezo na wadau wake.
Pamoja na mambo mengine program
hii itatoa fursa kubwa sana kwa wadau kuleta mawazo yao ili wizara iweze
kuwaingiza kwenye mnyororo wa thamani wa shughuli zake kwani wizara
inatamani ifanye kwa mlengo ambao wadau weke wanatamani ifanyike.
Progamu hii itazinduliwa rasmi
tarehe 14 Mwezi Februari mwaka 2017 hapa Jijini Dar es Salaam ambapo
itahushisha sekta ya Utamaduni na hapo baadaye mikutano hii inaweza
kufikiriwa na kufanywa kwa kanda. Mpango huu utahusisha pia Taasisi
zilizo chini ya wizara.
|
No comments:
Post a Comment