Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Wafanyakazi wa Halmashauri ya
wilaya ya Kondoa dc idara za Ulinzi,Madereva,watendaji Kata na vibarua
wanaolipwa kwa fedha za makusanyo ya mapato ya ndani wamemuomba waziri
wa Tamisemi George Simbachawene kunusuru kaya zao kwa kuingilia kati
suala lao la malimbikizo ya mishahara wanaoidai kwa miezi mitano sasa
ili kuwanusuru na hali ngumu ya kimaisha wanaokabiliana nao kwa sasa.
Wafanyakazi hao waliongea na
gazeti hili wilayani humo walisema kuwa wanakumbana ha hali ngumu ya
kimaisha inayosababishwa na wao kukosa fedha zao za mishahara kwa miezi
mitano sasa huku wimbo ukiwa ni suala lao lipo kwenye mchakato na miezi
inaenda.
Mmoja wa wafanyakazi aliekataa
kutaja jina kwa hofu ya kusimamishwa kazi kwenye idara ya ulinzi alisema
kuwa wamekuwa wakifuatilia fedha zao kwa kipindi kirefu huku wakiambiwa
mkurugenzi amekwisha saini dodoso la malipo yao lakini wao mpaka leo
hawajalipwa chochote hiyo imekuwa ikiwawiya vigumu katika hali za
kimaisha mjini.
Amesema kuwa mjini unakuwa
umepanga nyumba una watoto unasomesha wanahitaji chakula na mahitaji
mengine sasa unafikiria utaishi vipi kwa hali tunamuomba waziri Tamisemi
kuingilia kati kuweza kulipwa fedha zetu kwani mamlaka zote ngazi ya
wilaya wanalijua suala letu bila majibu wala kupata stahiki zetu tena
ambazo tunazivujia jasho usiku na mchana.
Kwa upande wake mmoja wa vibarua
amesema kuwa fedha zao wanazodai katika halmashauri hiyo imekuwa ni
usumbufu na kila wanapokwenda kwa Mhazini wa halmashauri madai yake
fedha hakuna fedha hivyo wao kuendelea kuishi katika hali ngumu ya
kimaisha na huku familia zikiwategemea.
“Sisi tunamuomba sasa waziri
simbachawene kulifuatilia suala letu kwani tunaimani na serikali ya
awamu ya tano katika kuwajali wanyonge na watu wa kipato cha chini hivyo
tunaamini atalishughulikia”aliongeza mfanyakazi huyo
No comments:
Post a Comment