Diamond
Platinumz amedai kuwa uhasama kati yake na Ali Kiba ulipikwa na chombo
kimoja cha habari kwa lengo la kumuondoa kwenye ramani ya muziki.
Bosi
huyo wa WCB amefunguka katika mahojiano na Lil Ommy wa Times FM, ambapo
amedai kuwa uhasama huo ulikuwa miongoni mwa mbinu za muda mrefu
zilizoshindwa za kutaka kumuua kimuziki.
Amesema
kuwa baada ya kugundua mbinu hiyo, alikutana na Ali Kiba jijini Nairobi
na akazungumza naye kuhusu hilo na wakakubaliana hakuna tofauti kati
yao.
Diamond ambaye anapromoti albam yake mpya ya ‘A Boy From Tandale’
alisema kuwa tofauti kati yake na Ali Kiba haiko kiuhalisia kwani
inatengenezwa na watu wasiomtakia mema na kukuzwa na mashabiki.
Aliongeza
kuwa njama na jitihada za kutaka kumuangusha kimuziki zilianza miaka
minne iliyopita lakini haziwezi kufanikiwa. Alisisitiza kuwa hakuna
anayeweza kumuua kimuziki akiwa hai, “labda unitoe uhai, lakini kuniua
kimuziki haiwezekani.”
Lil Ommy alitaka kujua kama nyimbo za Ali Kiba zitachezwa kwenye vituo vya Wasafi Radio na Wasafi TV.
“Bro
nisikudanganye, pale atachezwa kila msanii na yeyote mwenye talent
(kipaji). Hadi sasa pale watu wanabishana kuhusu slogan (kauli mbiu),
kuna wanaosema ‘Welcome Home’ na ‘Hii ni Yetu Sote’. Kwa hiyo hii ni ya
wasanii na haipo kwasababu ya matabaka,” alijibu.
Chibu
alisema kuwa ushikirikiano wa wasanii ndio utakaoendelea kuukuza muziki
wa Bongo Fleva na sio uhasama na ushindani usiokuwa na lengo zuri.
No comments:
Post a Comment