Waziri
wa Kilimo, Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuria mkutano wa 11 wa baraza la
taifa la Biashara uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuendeshwa
na Rais Dkt Magufuli.
Katika
mkutano huo Rais Magufuli aliwahitaji mawaziri hao ili waweze kutoa
ufafanuzi kuhusu maswala ambayo yameibuliwa na wafanyabiashara, lakini
mawaziri hao pamoja na Makatibu wao hawakufika licha ya kuwa walialikwa
na kupaswa kuwepo kwenye mkutano huo.
Kufuatia
kutokuwepo kwa viongozi hao, Rais Magufuli alimuuliza Waziri Mkuu
(Kassim Majaliwa) kama waliweza kuwaalika mawaziri hao na ndipo Waziri
Mkuu alipojibu kuwa walipata mualiko na walipaswa kuwepo kwenye mkutano
huo ingawa hakukuwa na taarifa yoyote ya wao kutokuwepo wala kutuma
wawakilishi wao.
"Kwa hiyo wa Kilimo na Mifugo mawaziri na Makatibu wakuu wote hawapo?............Wao sio wajumbe wa mkutano huu? Alihoji Rais Magufuli ndipo Mawaziri Mkuu aliibuka na kutoa majibu kwa Rais Magufuli.
"Mawaziri
wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na "kusupport" uchumi wetu wa
viwanda, kilimo ni "facilitater" (msimamizi) wa viwanda na Mifugo naye
pia ni wa viwanda walikuwa wapaswa kuwepo hapa kwa sababu walishapewa
taarifa wote"
No comments:
Post a Comment