Muigizaji
wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka na kuwaasa wasanii wenzake wa
Bongo movie waache kumlilia msanii mwenzao Steven Kanumba na badala yake
waenzi kazi zake.
Steven
Kanumba alikuwa msanii wa Bongo movie ambaye alikuwa ni mfano wa kuigwa
na kila msanii kwani uwezo wake wa kuigiza na ubunifu uliweza kwa kiasi
kikubwa kuifikisha tasnia hiyo mbali.
Ikiwa
zimepita siku kadhaa tangu tasnia hii ikumbuke siku ya kifo chake
ambayo inaitwa Kanumba Day, Aunty Ezekiel amefunguka na kusema sasa
kuomboleza kifo chake tu kumetosha.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Aunty Ezekiel amesema kuwa
mara nyingi wasanii wanapoadhimisha kumbukumbu ya kifo chake, wanakuwa
wanalia au wengine wanasononeka mara kwa mara hiyo inakuwa inazidi
kurudisha tasnia nyuma badala yake wasanii wakaze buti waweze kufika
alipokuwa amefika yeye.
"Najua
wazi uchungu upo lakini inabidi tuache sasa kulia badala yake
tujitahidi kufikia pale alipotuacha ili tuzidi kusonga mbele maana
tukisema kulia kila siku hatuwezi kufika tunapotaka hata siku moja”.
No comments:
Post a Comment